Kocha wa timu ya taifa Harambee stars Engin Firat yupo kwenye shinikizo la kutafuta matokeo bora katika mechi ya pili msimu huu ya kuwania tikiti ya kushiriki mashindano ya AFCON 2025 kutoka kwa mashabiki wa Kenya.
Kulingana na mashabiki ni mfumo wa kiufundi anaoutumia Firat kwenye kupanga kikosi chake ambacho anaonekana akiacha nje wachezaji muhimu ambao mashabiki wanadai huenda wangeleta matokeo bora.
Katika mechi iloisha sare tasa dhidi ya Zimbabwe Firat alionekana kuacha nje washambuliaji kama John Avire pamoja na Benson Omala ambaye msimu jana alikuwa mfungaji bora.
Kenya itakuwa inachuana na Namibia hiyo kesho katika taifa la Africa kusini ikiwa ni mechi ya nyumbani kwa Namibia ambao wanachangamoto ya viwanja katika taifa lao.

