TETESI ZA UHAMISHO MASHINANI (PWANI)

Huku dirisha la uhamisho likiwa bado lipo wazi katika ligi ya mkoa wa pwani hadi mwezi September tarehe 22 vilabu bado viko sokoni kuimarisha vilabu vyao kuelekea msimu ujao.

Klabu ya Kisumu Ndogo United inayotokea mji wa Malindi imeonesha nia ya kutaka kumsajili Bajeli Menza kutoka klabu ya Matano Mane youth kutoka eneo bunge la Ganze.

Winga huyo mchango kwa sasa bado ni mwanafunzi katika shule ya upili ya Vitengeni Baptist na huenda kusajiliwa kwake kukawa na kikwazo cha kupatikana uwanjani akihitajika Malindi.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Young Bulls ambaye kwa sasa yupo Ruiru Hotsters Samson Ndegwa anahusishwa na uhamsiho wa kuelekea katika klabu ya Mombasa All Stars. Taarifa zasema kuwa kiungo huyo amekamilisha taratibu zote za uhamisho kufikia sasa.

Hassan Mtengo licha ya kuhusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Bumbani Stars inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza msimu ujao, amethibitisha kuwa atasalia katika klabu yake ya sasa Young Bulls.

Beki huyo kisiki amesema kuwa anafurahia kusalia katika kambi ya Malindi High na yupo na matumaini ya kufanya kazi njema na mkufunzi mpya Ali Mwachaunga.