MBAPPE AANZA KWA UKAME

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Klyian Mbappe ameanza msimu kwa ukame wa mabao tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na mashabiki wengi wa soka la ulaya katika klabu yake mpya Real Madrid.

Mbappe katika mechi ya laliga yake ya kwanza katika uwanja wa Santiago Bernabou huko Madrid dhidi ya Valladolid alitoka katika mechi bila hata bao, mechi ambayo Real ilishinda kwa mabao 3-0.

Mabao katika mechi hiyo yalifungwa na federico valverde, Brahim Diaz pamoja na sajili mpya kinda Endrick wa Brazil ambaye alichukua nafasi ya mbappe kama ingizo la dakika za lala salama.

Mkufunzi wake Carlo Ancelotti amemkingia kifua Mbappe kwa kusema kuwa ni swala tu la muda na ataanza kufunga kama alivyokuwa wamoto Paris SG.