IKKAY GUNDOGAN AREJEA MANCHESTER CITY

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Ikkay Gundogan atarejea rasmi katika klabu ya Manchester City kutoka Barcelona.

Hii ni baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana kwenye uhamisho wa bila malipo kwa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 33.

Gundogan ambaye aliwahi kuwa naibu nahodha wa Manchester City anarudi katika klabu hiyo baada ya Pep Guardiola kukubali uhamisho huo awali akisema kwamba ni mchezaji mzuri sana na angefurahi iwapo angerejea.

Hayo yanajiri baada ya wiki hii Gundogan kutangaza kuwa amestafu soka la kimataifa na timu yake ya Ujerumani.