Shirikisho la soka fkf limemruhusu sasa Hussein Mohamed ambaye ni naibu mwenyekiti wa klabu ya Muranga Seal kuhudhuria kikao cha washikadau wa soka nchini kilichoratibiwa wikendi ijayo.
Kulingana na taarifa ni kuwa Muranga seal imetuma waraka wa kuitaka fkf imkubali Hussein kuwa mwakilishi wa klabu hiyo ya ligi kuu nchini.
Awali Fkf ilikuwa imemfungia Hussein kutoingia kwenye vikao vya fkf kwa kile walichokuwa wanataja kuwa sio mwanachama wa Muranga seal.
Hussein ambaye pia ni kati ya wakenya waliotangaza hadharani nia yao ya kupigania urais wa fkf mwaka huu alifungiwa mara kadhaa ikiwemo kikao cha mwezi Machi cha shirikisho.

