MCHEZAJI BORA WA FAINALI KILIFI NI MCHEZAJI HURU

Mchezaji bora katika fainali ya mashindano ya Dola Super Cup Ahmed Athman Shakur aliyewasilisha Kilifi South ilihoibuka mabingwa wa Dimba hilo katika kaunti ya Kilifi amethibitisha kuwa yeye kwa sasa ni. Mchezaji huru baada ya kuachana na klabu yake ya nyumbani Silver Bullets iliyoshuka daraja.

Akizungumza na Tama La Spoti amethitibisha kuwa kwa sasa hajapata taarifa zozote zinazomhusisha na klabu yoyote kwenye dirisha la Sasa la usajili.

Amepongeza ujio wa mashindano ya Dola katika kaunti ya Kilifi akihoji kuwa yameleta uchangamfu katika soka la mashinani.Ikumbukwe kwamba Shakur ni kati ya wachezaji wa timu ya Junju walioshinda mashindano ya kombe la Governor’s Cup katika kaunti ya Kilifi kwenye fainali ilopigwa katika uwanja wa chuo kikuu cha pwani mwezi April I mwaka huu.