HENRY ANAIMANI NA KIKOSI CHAKE

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwenye Olimpiki Thierry Henry anasema ana matumaini makubwa vijana wa Ufaransa wataibuka mabingwa kwenye mashindano hayo mwaka huu.

Ameyasema hayo kipindi ambacho Ufaransa inasubiri kucheza fainali jioni ya leo dhidi ya Uhispania.

Amesema kuwa wenyeji wa mashindano ya Olimpiki mwaka huu kumewasaidia pakubwa kuleta ushindani mkali katika kipute hicho.

Vile vile amewapongeza mashabiki na wananchi kwa kusema kuwa umoja wao na kuishabikia timu yao kumeisaidia pakubwa kuwa kati ya timu zinazoonyesha uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa mwaka huu.