MECHI YA NGAO YA JAMII YAPIGWA KALENDA

Klabu ya Gor Mahia imethibitisha kuwa mechi ya kufungua msimu ya Ngao ya jamii iliyokuwa inakutanisha klabu hiyo ya Kogalo na Police FC imepigwa kalenda

Mechi hiyo ilofaa kuchezwa tarehe 11 mwezi huu wa Agosti imeahirishwa mwa muda kutokana na shirikisho la fkf kusema kwamba wamekosa kupata kiwanja chenye hadhi ya kuandaa kipute hicho.

Gor Mahia wametoa taarifa hiyo huku wakizidisha maandalizi yao kwa msimu mpya wa 2024/2025 ambapo watakuwa pia wanashiriki katika mashindano ya Caf.

Kwa sasa Gor Mahia imeratibiwa kushiriki mechi za kirafiki kujiweka sawa dhidi ya vilabu vya hapa hapa Afrika mashariki.