Mkufunzi wa timu ya soka ya Magarini kaunti ya kilifi bwana Suleiman Bahero anasema kikosi chake kiko imara kuvaana na mpinzani yeyote katika mashindano yanayoendelea ya Dola Super Cup.
Akizungumza na Tama la spoti kupitia njiaya simu Bahero anasema uteuzi wa kikosi bora ndio umemfanya kuzidi kupata matokeo mazuri kwenye kipute hicho kufukia sasa na kuingia hatua ya semi fainali.
”Mimi nilianza kujitayarisha kitambo. Nimeandaa kikosi cha mauwano kwenye hiyo mechi ya kesho. Paps nakwambia wewe mwenye utajionea vipaji viko Magarini. Nimechagua kikosi bora ambacho hapo usipokula bao 5 umeponea” Alisema Bahero
Anasema ametoa wachezaji wake kutoka sehemu mbalimbali na amewaonya wapinzani wake Kilifi South katika semi fainali itakayochezwa kesho katika uwanja wa GFC wajitayarishe na upinzani mkali kutoka kwao.

