BUMBANI STARS YALALAMIKIA MINI LEAGUE

Mkufunzi wa klabu ya Bumbani Stars Mwaduka Bakari amesema kuwa hafurahishwi na jinsi usimamizi wa ligi za fkf ulileta mfumo wa kufanya vilabu vilivyochukua ubingwa wa ligi kama ya daraja la pili kwenda mini ligi badala ya kupanda moja kwa moja.

Kocha huyo anasema huo ni mfumo mbovu, na anasema Bumbani Stars walistahili kupanda moja kwa moja na wala sio kushirikishwa kwenye mini ligi jambo ambalo anasema si haki iwapo timu italemewa kwenye mashindano hayo…

Bumbani Stars na Ziwani Youth klabu iliulyomaliza katika nafasi ya pili msimu uliotamatika majuma kadhaa yalopita zitashiriki katika mini ligi hiyo ambayo bado Ratiba yake bado haijabainika.