Klabu ya Junior Fc kutoka kaunti ya Taita Taveta inalenga kufanya usajili kukiimarisha kikosi chao katika ligi ya daraja la pili kuelekea msimu ujao.
Kulingana na kocha wa klabu hiyo Zablon Mwale ni kuwa klabu hiyo iko kwenye mazungumzo na wachezaji watatu ambao watawasajili kabla ya msimu ujao kuanza.
Amedokeza kuwa baadhi ya wachezaji hao wanawakikisha shule ya Upili ya Dr Agrey katika mashindano ya kitaifa ya shule za upili katika kaunti ya Kisii, mashindano ambayo yameanza rasmi hii leo.
Junior FC ilishiriki ligi ya fkf daraja la pili kitaifa msimu uliopita kwa mara yao ya kwanza na ikiwa ndio timu ya tatu kutoka Taita Taveta katika ligi hiyo. Teita Estate pamoja na Kamtonga FC ndio vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo

