MSAMBWENI THREE YANG’AA KWALE

Timu ya soka ya msambweni 3 ndio mabingwa wa mashindano ya Dola Super Cup katika kaunti ya Kwale.

Hii ni baada ya kuichakaza timu ya Msambweni Two kichapo cha mabao 4-0 katika uwanja wa Ukunda Show ground.

Athman Bori ndiye aliibuka mshindi wa mchezaji bora katika mechi hiyo kwa kutia wavuni mabao 2 kwenye fainali hiyo iliyojaa mbwembwe na burudani.

Msamweni Four sasa wanasubiri kujua watachuana na nani katika mashindano ya kimkoa huku mashindanoya dola super cup yakiwa yameanza rasmi wikendi hii katika kaunti ya kilifi.

Mechi ya kwanza ilikuwa ni ile ya Kilifi Kaskazini dhidi ya Malindi A iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 katika uwanja wa pwani University siku ya jumamosi.