MOFA KUSHIRIKI NSL MSIMU UJAO

Klabu ya Rainbow Fc iliyokuwa inashiriki katika ligi ya kitaifa ya Super League imebainika sasa itashiriki katika ligi ya daraja la pili la Fkf.

Nafasi yao sasa imechukuliwa na klabu ya MOFA inayomilikiwa na nahodha wa timu ya taifa Harambe Stars Michael Olunga klabu ambayo msimu uliopita ilikuwa inashiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa.

Kati ya sababu za Rainbow kujiondoa kwenye ligi ya kitaifa ni kutokana na vikwazo vilivyoko kwenye ligi ambavyo ni pamoja na sheria mpya ya timu kutakikana kuwa na timu ya vijana, kocha mkuu wa timu anapaswa kuwa na cheti cha Caf kiwango cha B pamoja na timu husika kwenye Super League kuwa na timu ya kinadada.

Vile vile Rainbow imethibitisha ugumu wa kiuchumi hapa nchini umewafanya kushindwa kujisimamia katika ligi ya kitaifa ya Super League.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa Michael Olunga alitaka kuinunua Rainbow jambo ambalo halikufaulu kufanyika.

Hata hivyo Olunga analenga kununua klabu moja nchini Sweden ambayo imelemewa na fedha za kujidhamini kwenye ligi.