TEN HAG AREFUSHA MKATABA OLD TRAFFORD

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amerefusha mkataba wake na kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2026.

Hii ni baada ya mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mkataba huo baada ya dalili nzuri kutokea kutoka kwa viongozi kumkubali aendelee kuwa mwalimu wa The Red Devils licha ya tetesi zilizokuwa msimu ulipotamatika kuwa angefutwa baada ya fainali za kombe la FA.

Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Ajax FC mwenye umri wa miaka 54 mkataba wake Old Trafford ulifaa kutamatika mwakani lakini kutokana na kuwatafutia waajiri wake nafasi kwenye mashindano ya Europa msimu uliopita kupitia kushinda kombe kwa klabu hiyo baada ya ukame wa miaka sita wamempa nafasi nyingine ya mwaka wa ziada.

Bruno Fernandes ambaye kwa sasa anaiwakilisha timu yake ya Ureno kwenye mashindano ya Euro 2024 huko Ujerumani kwa sasa mazungumzo yanaendelea ya kuzidisha mkataba wake na Manchester United baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa angeibukia Bayern Munich majira ya joto.

Pia Manchester United haina mpango wa kumwachilia Marcus Rashford kuelekea msimu ujao licha ya tetesi zinazomhusisha kuelekea PSG kuchukua nafasi ya Klyian Mbappe aliyeenda Real Madrid.