Klabu ya Naivas Fc itashuka dimbani dhidi ya SOFAPAKA tarehe 6 mwezi Julai kutafuta nafasi ya kupanda ligi kuu ya FKF nchini kenya msimu ujao.
Hii ni baada ya kujipata katika nafasi nzuri ya kuelekea mashindano ya kufuzu baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi na alama 76.
Msimu wa FKF National Super League ulitamatika rasmi wikendi ilopita na Mara Suger walijishindia ubingwa wa kampeni hiyo.
Sasa Mara Suger na Mathare United waliomaliza katika nafasi ya pili wamefuzu moja kwa moja kufuzu kuingia KPL msimu ujao.

