WAZIRI NAMWAMBA ANA IMANI WANARIADHA

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba anatarajia Timu ya Kenya kuandikisha matokeo bora zaidi kuwahi kutokea katika Michezo ya Olimpiki watakapo shiriki kwenye makala ya mwaka huu jijini Paris, na hii ni kulingana na anavyoona maandalizi yao kufikia sasa.

Ababu ameyasema hayo kipindi ambacho alikuwa ameenda kuwapa vifaa na mavazi wachezaji wa timu hiyo jijini Nairobi ambapo anasema dhamira ya serikali ni kuhakikisha wanariadha hao wanaandaliwa vyema zaidi.

Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki nchini Paul Tergat pia ana imani kuwa timu ya Kenya itaandikisha matokeo mazuri mwaka huu.

Michezo hiyo ya olimpiki inatarajiwa kuanza rasmi mwezi Julai mwaka huu huku riadha ya kenya, raga ya Kenya Sevens na michezo mingine ikitarajiwa kushirikishwa katika mashindano hayo.