Baada Ya Kupata Tiketi Ya Kushiriki Kombe La Dunia La Fifa La U-17 Mwaka Huu Linalotarajiwa Kufanyika Huko Jamuhuri Ya Dominika Mwezi Oktoba, Serikali Kupitia Wizara Ya Michezo, Imeahidi Kusimamia Maandalizi Sahihi Na Ya Kina Kwa Junior Starlets, Ambayo Itashiriki Kwa Mara Ya Kwanza Katika Onyesho Hilo La Kila Baada Ya Miaka Minne. .
Baada Ya Kufikia Hatua Hiyo Muhimu, Timu Hiyo Inayoongozwa Na Mildred Cheche Imekuwa Timu Ya Kwanza Ya Kenya Kufuzu Kwa Onyesho La Kombe La Dunia La Fifa.
Kulingana Na Waziri Wa Vijana, Sanaa Na Michezo, Ababu Namwamba, Serikali Inajitahidi Kuwaweka Sawa Wasichana Hao Kuelekea Mashindano Hayo Ili Kuchochea Matokeo Mazuri Kwenye Ushiriki Wao Wa Kwanza.
Waziri Huyo Ametoa Wito Kwa Mashirika Ya Kibiashara Kujitokeza Kusaidia Kuinua Michezo Tofauti Nchini.
Rais Wa Shirikisho La Soka La Kenya (Fkf) Nick Mwendwa Amesema Wamependekeza Kwa Wizara Ya Michezo Kufikiria Kuipeleka Junior Starlets Nchini Uhispania Kwa Kambi Ya Mazoezi Kwani Timu Nyingi Ambazo Zimefuzu Kwa Mchuano Hiyo Pia Zimechagua Taifa Hilo Kwa Kambi Zao Za Matayarisho.

