SERIKALI YAJIVUNIA TALANTA HELA

Wizara ya michezo hapa nchini ikiongozwa na Ababu Namwamba inajivunia kuwa mradi  wa serikali wa Talanta Hela umeanza kuzaa matunda.

Ababu amethibitisha kuwa vijana wengi waliowakilisha Kenya na kuandikisha historia ya kufuzu kwa kombe la dunia wametokana na mpango wa Talanta Hela wa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19.

Swali kubwa linaloibuka kwa wachezaji na wananchi ni kuhusu mitihani ya kitaifa ambayo itafanyika  mwishoni mwa mwaka huu wasichana wengi wa Junior starlets wakiwa ndio mwanzo wamekita kambi uhispania kabla ya safari yao kwenda Jamhuri ya Domonika.

Rais wa shirikihso nchini Nick Mwemdwa anasema huenda wakalazimu wanafunzi hao kukosa mitihani hiyo na kuifanya baadaye baada ya mashidano ya kombe la dunia.