Shirikisho la soka hapa nchini Kenya FKF chini ya Nick Mwendwa rais wa shirikihso hilo linajivunia kuwa uongozi wa kwanza wa soka kuipeleka Kenya katika mashindano ya soka ya dunia.
Nick Mwendwa akizungumza baada ya kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Starlets waliofuzu kwa kombe la dunia anasema ni faraja kubwa kwao kama shirikihso kwa kupiga hatua hiyo.
Junior Starlets jana katika mechi ya marudiano na Burundi ilisajili ushindi wa mabao 2-0 na kufuzu kwa kuipiga Burundi mabao 5-0 baada ya raundi ya kwanza kusajili ushindi wa mabao 3-0 huko Addis Ababa ugenini.
Waziri wa michezo Ababu Namwamba kwa upande wake anasema serikali tayari ishaandaa sehemu ya kuipeleka Junior starlets kwa mazoezi ya lala salama kabla ya safari yao ya Domonican Republic tarehe 16 mwezi October kwa mashindano hayo.

