VILABU VYA FKF KILIFI VYAILILIA OFISI

Wito umetolewa kwa shirikihso la soka la FKF kuwa makini na wachezaji kusajiliwa na klabu zaidi ya moja, makocha wakilalamikia hali hiyo kuumiza baadhi ya vilabu.

Kulingana na mkufunzi wa klabu ya Beach Bay James Mkutano kutoka magarini kaunti ya Kilifi ni kuwa kipindi hiki ambacho misimu yaligi kubwa imetamatika kuna baadhi ya wachezaji wanakuja kashinani kwa ligi nyingine, jambo ambalo linasababisha ushindani ambao sio halali.

”Kwa sasa ligi iko mwishomwisho na kuna baadhi ya ligi zimeisha kwa mfano Div One. Sasa kuna wachezaji ambao wanasajiliwa na vilabu vingine wakiwa ni wachezaji wa vilabu vyao tayari. Hali hii ya udanganyifu inafanya hakuna ushindani halali.” Alisema mkutano

Vilevile Mkutano amemshauri mwenyekiti wa FKF katika gatuzi la Kilifi Dickson Angore kuzingatia kuvipa sapoti vilabu vya kaunti yake kwani sasa kwenye ligi ya daraja la pili vinapata ushindani mkubwa kutoka vilabu vya kaunti ya Mombasa ambavyo viko chini ya Lillian Kazungu.

Kwa sasa vilabu vya Kilifi kwenye msimamo wa ligi viko katika eneo hatari la kushuka daraja.

”Dicky anafaa atutetee sisi kama wanakilifi. Lillian kule Mombasa anatetea timu zake ilhali huku kwetu hatuna mtetezi. Misimu ijayo utaanza kuona Mombasa ndio imejaza ligi za Div 2 na Div One kisa sisi tunakosa watetezi.” Aliongeza Mkutano