Waziri wa Michezo Ababu Namwamba ameihakikishia timu ya raga ya wachezaji saba msaada mkubwa kutoka kwa serikali.
Ameyasema hayo baada ya kushuhudia timu hiyo ikifuzu kwa Msururu wa Sevens Duniani wa 2025 jijini Madrid Uhispania jumapili.
Waziri huyo amewasifu Shujaa, na kuahidi kuwa serikali itatumia rasilimali zaidi kuhakikisha wanadumisha hadhi yao ya msingi katika ligi hiyo kubwa duniani.
Shujaa wamerejea nchini rasmi na wanalenga kurejea katika mazoezi siku chache zijazo kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano ya Olimiki mwaka huu Paris Ufaransa, Kenya ikiwakilisha Afrika katika mashindano hayo.

