Ukosefu wa wachezaji wenye uzoefu katika kikosi cha Junior FC inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili ndio sababu kuu iliyopelekea klabu hiyo kutoka kaunti ya Taita Taveta kupigwa kichapo cha katika mechi mbili za ugenini wiknendi hii.
Junior Fc wanaoshiriki ligi hiyo katika msimu wake wa kwanza ilishuhudia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya SparkiYouth kisha wakapigwa tena na Ziwani Youth kichapo kama hicho katika mechi yake ya pili.
Zablon Mwale ambaye ni kocha mkuu wa kikosi hicho anasema matokeo hayo yakutomrithisha yalilazimishwa na kukosa wachezaji wa kutosha wenye uzoefu, hata hivyo amewapongeza vijana wake wachanga kwa kujitolea uwanjani.
Ameeleza kuwa ukosefu wa fedha katika timu hiyo ndio jambo ambalo limeondoa viaja wengi wenye uzoefu ambao sasa wameenda kusaka ajira kwengineno na kupunguza huduma zao uwanjani kiasi cha baadhi kukosa kufanya mazoezi.

