Mabao mawili ya mchezaji bora wa ligi kuu inchini Uingereza msimu huu Phil Foden na lile la kiungo wa uhispania Rodri ndio mabao yaliyotosha kuwapa ushindi wa mabao 3-1 Manchester City wanaoongozwa na mkufunzi Pep Guardiola dhidi ya Westham United katika uwanja wa Etihad.
Ushindi huo pia uliwahakikishia ubingwa wa kombe la EPL jana, sasa Cityzens wakiwa wamefikisha jumla ya makombe 8. Wameshinda kombe la EPL kwa miaka minne flululizo na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Norway Erling Braut Halaand akishinda kiatu cha dhahabu kwa mabao yake 27 msimu huu huku kipa wa klabu ya Arsenal David Raya akijishindi glavu ya dhahabu kwa kutoruhusu kufungwa bao katika mechi 16 msimu huu.
Ni rasmi sasa klabu ya Burnley, Luton City pamoja na Shiffeild United zimeshuka daraja msimu huu baada ya kuwa na msimu mbovu katika ligi kuu ya Uingereza.
Nafasi zao katika ligi zinachukuliwa na klabu ya Leicester City ambao wamepata nafasi ya kupanda pamoja na klabu ya Ipswitch lakini pia klabu moja kati ya klabu ya Leeds na Southhampton ambao sasa wanasubiri hatima yao wanapongangania tikiti ya kufuzu.

