Timu ya taifa ya kinadada wasiozidi umri wa miaka 17 hapa nchini Kenya Junior Starlets wamefuzu kutinga katika raundi ya nne na ya mwisho katika harakati zao za kutaka kuwakilisha Kenya katika mashindano ya kombe la dunia kwa wachezaji hao wachanga.
Wamefuzu baada ya kuipiga Ethiopia kichapo cha mabao 3-0 katika ardhi ya nyumbani kwenye uwanja wa Ulinzi Complex Annex.
Matokeo hayo sasa yanawafanya kukutana na Burundi katika raundi hiyo ya nne ambapo mshindi kwenye jumla ya mabao mengi moja kwa moja atakuwa amefuzu kucheza kombe la dunia, Junior Starlets wakiazimia kuwa timu ya kwanza kutoka Kenya kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia.
Junior Starlets walipata motisha wa kushinda mechi hiyo kutokana na uwepo wa mashabiki wengi, miongoni mwao akiwa ni waziri wa michezo Ababu Namwamba.

