UKOSEFU WA USHIRIKIANO UNAIPONZA MALINDI UNITED

Ukosefu wa ushirikiano baina ya baadhi ya viongozi wa klabu ya Malindi United pamoja na benchi la kiufundi lakini pia wachezaji ndio jambo ambalo limeishukisha pakubwa kiviwango klabu hiyo inayomilikiwa na mwakilishi wadi wa Malindi Rashid Odhiambo.

Hii ni kulingana na kocha Kassim Katana Tama La Spoti ilipofanya mahojiano ya kipekee na mkufunzi huyo katika mazingira ya uwanja wa Alaskan ambao ndio uwanja wao wa nyumbani.

Kocha Kassim ameshauri haja ya ushikamano katika klabu hiyo akam inalenga kuimarika katika siku za usoni la sivyo huenda ikasambaratika.

Kwa sasa klabu ya Malindi United tayari imetoa taarifa kukubali kuwa wameshuka daraja kutoka ligi ya Daraja la kwanza hadi la pili wanapoelekea msimu ujao, huku pia wakidokeza kuwa ratiba ya mechi mbili zilizosalia huenda wasiheshimu.