Timu ya kaunti ya Kilifi huenda ikasajili ubingwa wa mashindano ya KYISA katika mchezo wa Voliboli mwaka huu ambapo ndio waandaaji wa makala ya tisa ya michuano hiyo.
Akizungumza na Tama La Spoti katika uwanja wa Alaskan kocha mkuu wa kikosi cha kaunti hiyo Jimmy Ngala amepongeza hatua ya serikali kubuni timu ya kaunti ya mchezo huo hasa kwa wavulana kwa mara ya kwanza kabisa.
”Tunashukuru serikali ya kaunti kwa kukubali kujumuisha kikosi cha Voliboli katika mashindano haya. Tulijiimarisha na sasa tuna matumaini kikosi kiko vizuri na tutashinda ubingwa.” Alisema Ngalla
Kwa mantiki ya kuwa wenyeji Kilifi wanazidi kupata motisha wa mashabiki, na Ngala amewarai wakazi kujitokeza kwa wingi kujionea talanta lakini pia kushangilia vijana wao.
Mashindano ya KYISA yameanza rasmi leo michezo mitatu ndio imehusishwa ambayo ni pamoja na Soka, Mpira wa vikapu pamoja na Mpira wa wavu.

