KOMBE LA GAVANA LIMEZAA KIKOSI CHA KYISA!

Mashindano ya Governors Cup katika kaunti ya Kilifi ndio mashindano ambayo yamesaidia pakubwa upatikanaji wa kikosi kitakachowakilisha Kilifi katika mashindano ya KYISA mwaka huu, mashindano ambayo yalizinduliwa jana na yameanza rasmi hii leo.

Kulingana na kocha wa kikosi cha wavulana Rio Ngumao ni kuwa mashindano ya Governors Cup ambayo fainali zake zilipigwa jana katika uwanja wa chuo kikuu Pwani ni kuwa yameibua talanta za wachezaji wapya 15 ambao watajumuishwa kwenye kikosi cha Kilifi kwenye KYISA mwa ka huu.

Rio ameeleza imani yake na kikosi alichokabidhiwa rasmi kwa ajili ya shuhuli ya kupambania kaunti yake kushinda ubingwa wa makala ya tisa ya KYISA ambayo Kilifi ndio waandaaji.

Mashindano ya KYISA kwenye soka ni katika uwanja wa shule ya upili ya Malindi High, Basket Ball ikichezwa katika uwanja mpya wa Cleopatra Malindi na Voliboli mechi zikipigwa katika uwanja wa Alaskan.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *