Mwenyekiti wa shirikisho la soka katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi bwana Tom Lango amethibitisha kuwa mechi kati ya klabu ya Blue Stars dhidi Goshi United lakini pia ile ya St Clement dhidi ya Airmen zimepigwa kalenda hadi wiki ijayo huku mechi ya Drillers dhidi ya OXFORD ikipelekwa hadi Jumapili ili kupisha muda zaidi wa vilabu kujitayarisha.
Vilevile Lango amesema kuwa amefurahishwa na jinsi vilabu vimejitahidi kulipa ada ya usajili msimu huu huku kukiwa na matumaini ya kupigwa jeki na mbunge wa Malindi Amina Mnyazi haswa katika hela ya kujiandikisha.
Lango ametoa hakikisho kuwa msimu huu vilabu kutakuwa na tuzo za wachezaji bora pamoja na kipa bora toafuti na msimu uliopita ambapo kulikuwa na changamoto ya kutuzwa mabingwa.
”Msimu huu mwishoni lazima kutakuwa na tuzo kwa wachezaji waliofanya bora kwani tunajipanga vilivyo. Msimu huu tuna matumaini ya kupata udhamini kutoka kwa mbunge wetu wa sasa Amina Mnyazi” Alisema Tom.

