Kisumu Ndogo United hata kama ndio mwanzo imerejea katika ligi za FKF baada ya kukaa nje kwa muda mrefu msimu huu itaonyesha heshima yao kwenye ligi kwa kuandikisha matokeo bora au hata kupanda ligi msimu huu.
Hii ni kulingana na Ali Best ambaye ni kiongozi wa klabu hiyo kutoka mji wa Mlaindi kaunti ya Kilifi klabu inayoshiriki ligi ya mkoa kwa sasa.
”Ukiangalia hii timu ni ya juzi sana lakini imekuja kwa kishindo. Zamani Kisumu Ndogo United ilikuwa lakini ikaja kusambaratika wakati wachezaji walitokatoka lakini sasa tumekusanya wachezaji takriban 40 ili kuunda hii timu upya na tunashukuru tuko katika ligi ya mkoa. Msimu huu tunapania kupanda au kumaliza katika nafasi za juu kwenye ligi.” Alisema Ali
Wikendi hii Kisumu Ndogo United ilionyeshwa kichapo cha aibu cha mabao 4-0 dhidi ya Matano Mane Youth katika uwanja wao wa nyumbani Alaskan.

