THOMAS PARTEY KUANZA LEO, NDOVU AKIPIGA PUMZI ZA KUPANDA MTINI

Huenda Thomas Partey akaanza katika kikosi cha Gunners jioni ya leo ambapo watakuwa wanalenga kurejea kileleni mwa jedwali la ligi kuu uingereza baaada ya kupigwa breki wikendi ilopita katika sare tasa dhidi ya klabu ya Manchester City huko Etihad.

Arsenal inayoongozwa na kocha Mikel Arteta itakuwa nyumbani dhidi ya klabu ya Luton City ambao watakuwa wakicheza na taharuki kulingana na msimamo wao katika jedwali kwenye ligi ambapo wako katika hatari ya kushuka daraja.

Kwa sasa Arsenal inasimama katika nafasi ya pili na alama 65 alama mbili nyuma ya vinara Liverpool walio na alama 67 na hii ni baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Brighton siku ya jumapili.

Mechi mbili zaidi za ligi kuu uingereza zimeratibiwa jioni ya leo ambazo ni pamoja na Brighton watakaokuwa wanacheza dhidi ya Brentford huku Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wakimenyana na Aston Villa.