ANGELA OKUTOYI AANDIKISHA HISTORIA

Mchezaji maarufu wa tenisi nchini Kenya Angella Okutoyi sasa ni rasmi kuwa amefuzu kwa mashindano  ya Olimpiki ya Paris Ufaransa, baada ya kunyakuwa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Afrika mjini Accra, Ghana.

Okutoyi, ambaye 2022 aliweka historia kwa kushinda taji la Wimbledon kwa kitengo cha wachezaji wawili kwa chipukizi, aliwazaba Lamis Al-Hussein wa Misri 6-2, 6-4 na kushinda taji la Afrika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ameweka historia kama mwanamke wa kwanza Mkenya kushinda taji hilo la kifahari baada ya takriban nusu karne, tangu ushindi wa Jane Davies mwaka wa 1978.