WACHEZAJI WAKONGWE KUNUFAIKA

Waziri wa michezo hapa nchini Kenya Ababu Namwamba amewahakikishia wachezaji wa zamani hasa wanariadha huenda wakanufaika na bima ya afya iwapo sheria itapitishwa.

Ameyasema hayo katika mazishi ya Henry Rono ambaye ni mwana riadha wa zamani akidokeza kuwa bima hiyo huenda ikasaidia pakubwa kwenye kusherehekea mabingwa wa zamani ambao waliwakilisha taifa hili zama zao.

Ametoa hakikihso kuwa serikali inampango wa kuongeza mgao wa kifedha unaotumika kama kiinua mgongo kwa wakongwe.

Vilevile ameshauri wanariadha ambao wanawakilisha taifa hili mwezi aprili katika mashindano ya Olimpiki huko Paris Ufaransa kupambana kushinda mataji kwa heshima ya Henry Rono na Kelvin Kiptum walioaga dunia mwaka huu.