WITO WATOLEWA KWA KAUNTI KUPIGA JEKI MCHEZO WA ‘SKATTING’

Serikali ya kaunti ya Kilifi sasa imetakiwa kujenga viwanja zaidi vya michezo ya kuteleza  kupitia kwa viatu vya magurudumu maarufu kama Sketting   ili kunufaisha vjana wapenzi wa mchezo huo mjini Malindi.

Kulingana  na Kocha mkuu wa mchezo huo mjini Malindi Joseph Njenga tayari jumla ya vijana 300 wamejiunga na mchezo huo kufikia sasa tangu mchezo huo kuanza mjini Malindi.

Njenga anahoji kuwa mchezo huo unalenga kukabiliana na maovu y Watoto  katika jamii ikiwemo ulanguzi wa mihadarati na ngono za mapema miongoni mwa vijana.

Amesema kuwa tayari mipango ya mashindano ya mchezo huo imekamilika na kwamba jumla ya shule 10 kutoka Malindi zitashiriki huku klabu tatu kutoka Mombasa zikitarajiwa kushiriki pia .