JOTA NA KLOPP WASHINDA TUZO ZA MWEZI

Mkufunzi wa klabu ya Liverpool kule Uingereza ndiye mkufunzi bora wa mwezi January. Hii ni baada ya Liverpool kuwa na kiwango kizuri chini ya uongozi wake mwezi huo wakishinda mechi tatu za ligi mwezi huo kwa kufunga mabaomengi.

Diogo Jota ndiye mchezaji bora wa mwezi January mwaka huu. Hii ni baada ya mchezaji huyo wa Liverpool na Ureno kuonyesha kiwango bora alipovaa viatu vya Mo Salah Aliyekuwa afrika kwa mashindano ya AFCON.

Amehusika pakubwa kwenye kuipiga Newcastle, Chelsea pamoja na Bournemouth kwenye mechi za ligi.

Msimu huu amefunga mabao 9 na kutoa assists mbili katika ligi kuu nchini Uingereza.