BIDCO UNITED YALALAMA

Mkufunzi wa klabu ya BIDCO Fc Athony Akhulia amelalamikia maamuzi mabaya ya refa wa katikati ya uwanja akitaja kuwa ndio chanzo cha wao kupoteza mchuano wao dhidi ya Bandari FC wiki hii kwa kichapo cha mabao 2-1.

Ametishia kuwa silisha lalama zake kwa maafisa wa FKF kudadisiwa vyema akihoji kuwa kuna maonevu mengi katika ligi jambo ambalo linafanya vilabu kukosa matokeo mazuri kihalali.

Amelalamikia penalty isioyuwa ya haki waliyopewa Bandari baada ya mchezaji wao Francis Oduor kuangushwa katika kisanduku na Umar Kasumba.

Amesema lalama anazotuma sio kuwa mechi ifutiliwe mbali au wapewe alama lakini ni kuona kuna mabadiliko katika ligi hiyo. Hata hivyo anasema vijana wake wa Thika wanazidisha mazoezi yao kwa ajili ya mechi dhidi ya Mathare United wikendi hii.