Rais wa wa taifa la Nigeria amewazawidi wachezaji wa timu ya Super Eagles waliowakilishataifa hilo katika mashindano yalotamatika wikendi ilopita ya Afcon huko Ivory Coast.
Taarifa zasema kwamba rais Bola Ahmed amewapa utambuzi wa Member of the Order of the Niger ambayo ni tuzo kati ya tuzo kubwa za taifa ambazo raia wa taifa hupewa na serikali iliyopo mamlakani.
Mbali na hiyo rais amewapa kila mchezaji wa super eagles ardhi na nyumba kama njia moja ya kuwapongeza kwa kufika fainali hata kama walipoteza kwa Ivory Coast.
Super Eagles walipigwa na Ivory coast kichapo cha mabao 2-1 na rais Bola ametaja kwamba walionyesha uzalendo zaidi licha ya kupoteza katika fainali ambayo ilionyesha kuwa na ushindani mkali.

