Watu wanne ambao walikuwa wamezuru katika boma la mwanariadha Kelvin Kiptum kabla ya kifo chake walifika katika ofisi za DCI jana kuandikisha taarifa kamili kuhusu ziara yao na Kiptum baada ya baba mzazi wa Kiptum kuthibitisha kuwa watu hao walizuru kwao na hakuwa anawafahamu na walifaa kuchunguzwa.
Taarifa zasema kwamba wanne hao walikuwa kwa Kiptum kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara kuhusu mkataba na kampuni ya kichina inayohusisha Kiptum kufanya mauzo kupitia riadha zake.
Kwa sasa wanne hao wako huru huku uchunguzi zaidi ukiendelea. Mwili wa marehemu Kiptum umehifadhiwa huku maandalizi ya mazishi yakiendelea na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 mwezi huu.
Kiptum alifariki Jumapili 11/02/2024 katika ajali mbaya barabarani akiwa na mkufunzi wake mrwanda Gervais Hakizimana.

