Rafiki Kavoi mchezaji anayewaniwa sana na vilabu katika ukanda huu wa pwani ni rasmi sasa amethibitisha kuwa yeye atasalia kuwa mali ya Malindi United klabu inayomilikiwa na mwakilishi wadi wa Malindi Rashid Odhiambo hadi mwisho wa msimu.
Kulingana na Kavoi ni kuwa ataamua mustakabali wake kamili mwisho wa msimu ila kwa sasa yuko malikini kumaliza msimu vizuri. Hata hivyo kuna tetesi zinazomhusisha kujiunga na klabu ya Bandari Youth inayoongozwa na kocha Alex Shikhanga.
Vile vile Kavoi ametuma wito kwa vilabu kuwaachilia wachezaji kwa wakati wanapotaka hifadhi mpya katika vilabu vingine akisema kwamba kucheleweshwa au kutoachiliwa huvunja morale wa mchezaji. Hata hivyo anasema kwamba mbali na Mlaindi United, amethibitisha kuwa ni kweli wachezaji huwa wananyimwa fursa ya kuhamia vilabu wanavyotaka.

