Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Harambe Stars Denis Oliech anasema haridhiki na jinsi ambavyo wakongwe wa soka katika taifa hili wanachukuliwa na shirikihso la soka na serikali kwa jumla.
Ansema kwamba katika mataifa mengibne ya Afrika hasa Magharibi mwa afrika malegendari wanathaminiwa sana na huhusishwa katika mipango ya shirikihso la soka katika mataifa husika tofauti na ilivyo Kenya.
Ameyasema hayo akiwa Ivory Coast ambako amealikwa kuwa kati ya wakongwe wa soka la bara afrika ambako pia ameshirkihswa katika mechi ya kirafiki ya kuchangisha fedha za kujenga viwanja na miundo msingi mingine mashinani.
Oliech amedokeza kwamba huenda Kenya na afrika mashariki kwa jumla ikanyanganywa fursa ya kuandaa Afcon mwaka 2027 iwapo haitaonyesha kusonga katika maandalizi kabambe ndani ya miaka miwili ijayo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa CAF.

