KOCHA WA IVORY COAST EMERSE FAE AWATAKA TEMBO KUMAKINIKA

Kocha wa muda wa Ivory Coast Emerse Fae anasema timu yake lazima isalie na unyenyekevu baada ya ushindi wao mkubwa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Senegal katika hatua ya 16 bora.

Wenyeji wa michuano hiyo waliwaondoa mabingwa hao watetezi kwa mikwaju ya mafuta 5-4 siku ya Jumatatu kufuatia sare ya 1-1 baada ya muda wa ziada na kutinga robo fainali.

Ushindi huo ulileta mabadiliko makubwa kwa Ivory Coast, ambao walistahimili hatua mbaya ya makundi ambapo walishindwa mara mbili, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 4-0 na Equatorial Guinea katika hatua za makundi.

Huku wakiwa wamefuzu hatua ya robo fainali, Fae amesisitiza kuwa timu haiwezi kubebwa na matokeo hayo kwani kuna mechi ngumu zaidi zinazokuja kwenye robo fainali.

Baada ya kuleta mabadiliko makubwa na bahati nzuri, Fae anaonekana kudhamiria kuhakikisha kuwa mauaji haya makubwa ni mwanzo tu huku Tembo wakitafuta sifa zaidi kwenye AFCON