Mkufunzi wa sasa wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ni kati ya wakufunzi ambao wanafuatiliwa kurithi mikoba ya Xavi Hernandez wa klabu ya Barcelona ambaye analenga kujiuzulu mwisho wa msimu huu.
Arteta sasa anaungana na mkufunzi Jergen Klopp anayeachana na Liverpool mwisho wa msimu pamoja na Julian Nageslman ambao wanawania nafasi hiyo.
Hayo yanajiri taarifa zikisema kwamba Arteta analenga kujiuzulu ukocha wa Gunners licha ya kusalia na miezi 18 katika kandarasi yake ya sasa pale Emirates ili achukue nafasi ya kuongoza Barcelona.
Mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Hansi Flick ni kati ya wakufunzi wengine wanaotajwa kuwania kumrithi Xavi Hernandez pale Barcelona.

