MKOMBOZI FC KUKAMILIKA KARIBUNI HUKO MAGARINI

Mbunge wa eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Harry Kombe anasema kwamba harakati za kuanza kuifufua mkombozi fc zinaendelea baada ya kusaka talanta za wachezaji mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na Tama La Spoti , Harry Kome anasema lengo lake ni kuanza kuiweka kambini timu hiyo ambayo inajumuisha wachezaji waliochaguliwa kutoka timu na maeneo mbalimbali ya magarini huku akiwa na azma ya kuimarisha michezo katika eneo hilo.

”Kufikia Disemba timu ya Mkombozi FC ilikuwa tayari tunakamilisha kuiunda lakini mpaka sasa bado hatujaiweka kambini kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja.” Alisema Harry

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa soka katika eneo hilo wanazidi kutoa wito kwa mbunge kwenda mashinani mwenyewe kusaka talanta baada la kutuma watu wanaompotosha.

Hapi Kaingu ambaye ni mkufunzi wa Lubumbashi FC ni kuwa talanta zipo kwa sana mashinani lakini huenda zoezi la mbunge huyo likapata changamoto iwapo hatafika mashinani.