DROGBA ALALAMA, IVORY COAST YATIA AIBU

Nguli wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba amekiri kuwa kuna tatizo kubwa katika kikosi cha timu ya taifa akihoji kuwa matokeo yanayoonekana katika dimba la Afcon yanadhalilisha taifa hilo kwa kile anachokitaja kwamba ni aibu kuona timu inapigwa mabao mengi ilhali ndio waandaaji wa mashindano haya.

Ameyasema hayo baada ya jana kurabishwa kichapo cha kihistoria cha mabao 4-0 dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Kwa sasa Ivory Coast iko katika nafasi ya tatu katika kundi lao na maombi yote ni iwapo watamaliza kama timu bora ya tatu ambazo zitafuzu kuingia 16 bora.

Timu ya taifa ya Cape Verde pamoja na Misri ndio timu za hvi punde zaidi kufuzu kwa afcon katika hatua ya 16, katika mashindano ya kombe la afcon yanayoendelea kwa sasa huko Ivory Coast. Licha ya wawili hao kupiga sare ya mabao 2-2.

Mataifa mengine ambayo tayari yashafuzu ni Super Eagles ya Nigeria, Equatorial Guinea pamoja na mabingwa watetezi Senegal.