Wito umetolewa kwa mbunge wa eneo bunge la Magarini Harry Kombe kuboresha michezo katika eneo hilo ili kuinua viwango vya wachezaji mashindano. Hapi Kazungu ambaye ni mkufunzi wa klabu ya ligi ya kaunti Lubumbashi Fc amesema kwamba eneo la Magarini limebaki nyuma kimichezo tofauti na sehemu nyingine akihoji kwamba michezo imesaidia vijana wengi kuepuka kutenda maovu katika jamii.
Mkufunzi huyo ametoa wito wa kuundwa angalau kwa timu ambayo inawakilisha eneo bunge hilo katika ligi kubwa za kitaifa.
Mkufunzi Hapi ameongeza kwamba kwenye suala la timu ya Mkombozi ambayo inatarajiwa kuundwa na mbunge huyo wahusika waje mashinanim kusaka talanta tofauti ya kukaa maofisi, akihoji viwanjani ndio talanta zinaonekana.
Mechi ya daraja la pili ambayo ilikuwa imeahirishwa kuchezwa wikendi ilopita ya Kamtonga Fc dhidi ya Mariakani Fc itachezwa leo mwendo wa saa tisa huko Kamtonga katika kaunti ya taita taveta.
Matokeo ya mechi za wikendi hii kwenye ligi ya daraja la pili kitaifa ni kuwa Malindi Progressive katika uwanja wao wa nyumbani walipigwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Ziwani Youth.
Juniour FC vs Silver Bullets 0-1
Beach Bay vs Shimanzi 1-1
Kishada vs Samburu Lions 2-1
Inter Dabaso vs Teita Estate 3-1

