Mshambuliaji wa klabu ya Mofa inayomilikiwa na Michael Olunga mwite Alex Mwalimu ametoa taarifa kuwa klabu ya Mofa ni klabu sahihi kwake katika safari ya soka ya kuichezea timu ya Taifa Harambee Stars.
Ameyasema hayo akiwa kambini huko Homa Bay baada ya kukamilisha usajili wake mwezi huu wa January ambapo hadi kufikia sasa amecheza mechi moja pekee katika klabu hiyo inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza kitaifa.
Vilevile amemshukuru wakala wake Kaka Jabali kwa kumwezesha katika juhudi za kujiunga na klabu hiyo katika mkoa wa Nyanza.
Mwalimu ametoa shukrani zake kwa mashabiki zake lakini pia viongozi wa michezo katika kaunti ya Kilifi wakiwezo waziri, afisa mkuu wa michezo pamoja na gavana GeDION Maitha Mungaro.

