Waziri wa michezo Ababu Namwamba anasema ako na matumaini makubwa kwamba Kenya itashiriki mashindano ya Afcon mwaka 2025 baada ya mashindano ya mwaka huu Kenya kukosekana kutokana na kukosa kushiriki mashindano ya kufuvu baada ya kufungiwa na fifa.
Hata Hivyo ababu amewapongeza majirani Tanzania kwa kufunzu kwa mashindano ya mwaka huu akisema kuwa ni juhudi kubwa waliweka kufika hatua hiyo.
Ababu anasema kwamba Kenya kwa sasa inazidisha maandalizi ya Afcon mwka 2027 aksiema kwamba watayaandaa kwa kuwa wanatayarisha miondo mbinu ikiwemo viwanja vya hadhi ya FIFA.
Waziri huyo ameongeza kwamba kwa sasa wanawasiliana kwa ukaribu sana na CAF na amedokeza kuwa analenga kufanya kikao na viongozi wa shirikisho hilo ili kufanya ukaguzi wa maendeleo katika azma ya kujitayarisha kwa mashindano ya Afcon. Akiongeza kuwa kwa sasa Kenya inafuatilia kwa ukaribu sana mashindano ya AFCON huko Ivory Coast wakijifunza.

