Kocha mkuu wa Young Bulls, Ali Said Gaucho, ameondoka katika klabu hiyo ya FKF Division One yenye makaazi yake mjini Malindi kwa wiki moja sasa.
Gaucho ametaja kuna baadhi ya vitu ambavyo hakuvielewa baina yake na uongozi hivyo basi kulazimika kufunga virago. Kwa sasa, anahusishwa na kutua Malindi United ingawa dili hilo haliko wazi.
Coach Shaffi, ndiye atakayerithi mikoba ya kuinoa Young Bulls. Shaffi pia amewahi kuzinoa Congo Boys ikiwa KPL, Kilifi Combine na Magarini Combine zote zikiwa NSL.
Hayo yanajiri baada ya Malindi United inayoongozwa na kocha Elly Katana kupigwa bao 7-0 na Fortune Sacco wikendi ilopita. Mkufunzi Elly hata hivyo amethibitisha kuwa kuna wachezaji wengi katika kikosi chake ambao walikuwa wamekosekana baada ya likizo za Krismasi na Mwaka Mpya na bado hawajarudi.

