TUTAMALIZA NNE BORA – SILVER BULLETS

Meneja  wa timu ya Silver Bullets klabu inayoshiriki ligi ya FKF daraja ya pili kitaifa yenye makaazi yake eneo la vipingo ndani ya kaunti ya kilifi Ibrahim Chai ametaja ukosefu mazoezi  tosha kuwa chanzo cha wao kutoka sare tasa  na klabu ya Malindi Progressive Academy inayonolewa na mkufunzi Nero Chishenga.

Hata hivyo amesema wanarejerea mazoezi kambambe huku akiwa analenga kumaliza nafasi ya 4 bora ifikapo mwishoni mwa msimu huu ambao wanashiriki.

”Tuko na imani ya kumaliza katika nafasi ya nne bora msimu huu hata kama ndio wetu wa kwanza. Tunazidi kujiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi zijazo. Matokeo ya wikendi hii na Malindi Progressive Academy yalikuwa sare vile kutokana na baadhi ya wachezaji wangu hawakuwa wameiga tizi za kutosha” Alisema Chai

Mkufunzi huyo pia amekiri kuwapoteza wachezaji wawili muhimu ambao wanarudi shuleni ingawa ameonyesha kutokuwa na wasiwasi wowote kwa vile tayari ashapata wachezaji wa kuwarithi nafasi hizo.