MICHEZO IMESAIDIA PAKUBWA WAKATI WA LIKIZO – FKF

Visa vya vijana wenye umri mdogo kujihusisha na magenge ya uhalifu pamoja na utumizi wa mihadarati hasa kipindi cha likizo za Krismasi kutokana na vijana hao kuhusishwa sana katika michezo mbalimbali.

Mwenyekiti wa FKF katika gatuzi la Kilifi Dickson Angore amesema kwamba vijana wengi walishirikishwa sana katika mashindano mbalimbali msimu huu ambao umetamatika huku akithibitisha kuwa wamekuwa wakipewa hamasa kuhusu jinsi ya kujiepusha na mihadarati pamoja na uhalifu.

Vile vile Angore amesema kuwa mashindano ya msimu wa likizo wakati huu umesaidia sana kupungua kwa mimba za mapema hasa miongoni mwa wasichana kutokana na kwamba pia wamehusishwa katika michezo.