Klabu ya Beach Bay inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi inalilia udhamini ili kufadhili mechi zake.
Kulingana na MKufunzi James Mkutano ni kuwa ukata wa kifedha ni kati ya changamoto zinazowakabili kwa sasa jambo ambalo ana hisi limekuwa likivunja morale wachezaji wake.
Mkutano ametuma wito kwa washikadau mbalimbali lakini pia wadhamini kujitokeza na kuidhamini klabu hiyo ambayo dhiyo klabu ya pekee inayocheza ligi kubwa kutoka eneo zima la Magarini.
Ameyasema hayo baada ya jana kusajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Lubumbashy FC katika michuano ya OmarMshamu inayoendelea Magarini kwa sasa. Mabao katika mechi hiyo yalifungwa na Andrea Ngala pamoja na Kwicha Temo yote katika kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kuisha sare tasa

